DRC-UPINZANI-SIASA

Tshisekedi na Kamerhe wakataa uteuzi wa Fayulu kama mgombea wa upinzani DRC

Martin Fayulu (katikati) ateuliwa rasmi mgombea pekee wa upinzani katika uchaguzi wa urais wa Desemba 23 nchini DRC. Uamuzi uliochukuliwa huko Geneva na viongozi wakuu saba wa upinzani, Novemba 11, 2018.
Martin Fayulu (katikati) ateuliwa rasmi mgombea pekee wa upinzani katika uchaguzi wa urais wa Desemba 23 nchini DRC. Uamuzi uliochukuliwa huko Geneva na viongozi wakuu saba wa upinzani, Novemba 11, 2018. Fabrice COFFRINI / AFP

Felix Tshisekedi na Vital Kamerhe, viongozi wakuu wawili wa upinzani nchini DRC ambao walisaini kwenye mkataba wa uteuzi wa Martin Fayulu kama mgombea wa upinzani huko Geneva siku ya Jumapili, wameamua kujitoa kwenye makubaliano hayo.

Matangazo ya kibiashara

Kiongozi wa chama cha kihistoria cha upinzani cha UDPS, Felix Tshisekedi, alisema siku ya Jumatatu kuwa atajiondoa kwenye makubaliano aliyotia saini siku moja kabla na viongozi wengine wakuu sita wa upinzani kwa uteuzi wa mgombea mmoja wa upinzani katika uchaguzi wa urais uliopangwa kufanyika tarehe 23 Desemba nchini DRC.

Kwa upande wake, Vital Kamerhe kutoka chama cha UNC, amelaani njama zinazofanywa na wenzake wa upinzani na kukiuka mkataba ulio tiliwa saini siku ya Jumapili. Alitangaza pia kwamba anajiotoa kwenye mkataba huo.

"Nilidhani nilifanya vizuri kwa kuweka tofauti zetu kando na kumteua mgombea mmoja atakaye wakilisha upinzani katika uchaguzi wa Desemba 23, lakini mumeona vitimbi vya baadhi ya wenzetu." Kwa mtu mwenye busara, ninaweza kurejelea hatua yangu na kujiondoa kwenye makubaliano tuliofikia, "Felix Tshisekedi ameiambia VOA Afrique.

Uteuzi wa Fayulu ulizua sintofahamu kwa wafuasi wa Felix Tshisekedi na Vital Kamerhe ambao walipewa nafasi kubwa ya kuteuliwa kwenye nafasi hiyo kama mgombea wa upinzani kulingana na uchunguzi wa hivi karibuni.

"Sisi katika chama cha UDPS tunaamini kwamba suala hili la mgombea lilitengenezwa na serikali ili upinzani ushindwe katika uchaguzi ujao. Lakini tunajua kwamba hata kwa wagombea wawili au watatu, mgombea wa chama tawala na washirika wake hawezi kushinda upinzani pamoja na mbinu wanazofanya ili kushinda uchaguzi huo. Uchunguzi wa hivi karibuni unaonyesha, "amesema Tshisekedi.

Kwa upande wake, Martin Fayulu anaamini kuwa bado wenzake wa upinzani wanaendelea kumuunga mkono zikiwa zimesalia siku 10 kabla ya kuanza kwa kampeni za uchaguzi wa urais na wabunge uliopangwa kufanyika Desemba 23, 2018.