DRC-USALAMA-EBOLA

Ukosefu wa usalama na Ebola vyasababisha mdororo wa uchumi Mashariki mwa DRC

Timu inayopambana dhidi ya mlipuko wa ugonjwa wa Ebola katika Hospitali ya Bikoro nchini DRC.
Timu inayopambana dhidi ya mlipuko wa ugonjwa wa Ebola katika Hospitali ya Bikoro nchini DRC. REUTERS/Jean Robert N'Kengo

Ukosefu wa usalama wa kutosha na ugonjwa wa Ebola vinaendelea kuathiri maeneo mengi ya mashariki mwa DRC na kusababisha mdororo wa uchumi katika mkoa wa Kivu Kaskazini.

Matangazo ya kibiashara

Mkoa wa Kivu Kaskazini ambao unaendelea kukumbwa na mauaji ya raia, bado unaendelea kukabiliwa na ukosefu a usalama, huku raia wengi wakicha shughuli za kilimo kwa kuhofia usalama wao.

Shirikisho la makampuni nchini DRC na mashirika ya kiraia katika eneo hilo wameomba serikali kupunguza kodi ili kuwarahisishia wakaazi wa mji wa Beni kupata bidhaa mbalimbali mahitajio.

Katika soko kuu, hata katika maduka, wafanyabiashara wanalalamika wakisema: ". Hakuna wanunuzi"

"Mara nyingi wateja wetu wanakuja wakitokea Kinshasa, Goma na Kisangani, lakini hawaji tena kwa sababu ya mauaji, "alisema Marceline Kavira, mfanyabiashara katika soko kuu la Beni." Ni vigumu kwenda kutafuta bidhaa kwa sababu ya ukosefu wa usalama barabarani. Ghala ziko tupu, wakati hapo awali tulikuwa tukikosa seheu za kuhifadhi bidhaa zetu, "amesema, kwa mujibu wa VOA Afrique.

Kulingana na ripoti ya tarehe ya tarehe 11 Novemba 2018 ya Shirika la Afya Duniani (WHO), idadi ya watu waliofariki dunia kutokana na ugonjwa wa Ebola imefikia 209 mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.