AFRIKA KUSINI-SIASA

Waziri wa Mambo ya Ndani ajiuzulu Afrika Kusini

Malusi Gigabakatika mkutano na waandishi wa habari, Pretoria.
Malusi Gigabakatika mkutano na waandishi wa habari, Pretoria. REUTERS/James Oatway

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Afrika Kusini Malusi Gigaba ameamua kujiuzulu kwenye nafasi yake baada ya video ikimuonesha akijichua kusambaa kwenye mitandao ya kijamii nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Ofisi ya rais nchini Afrika kusini imethibitisha taarifa hiyo uya kujiuzulu kwa Malusi Gigaba.

Rais Cyril Ramaphosa amesema kupitia ukurasa wake wa Twitter kwamba amepokea barua ya kujiuzulu kutoka kwa Malusi Gigaba, na kukubali uamuzi wake.

Katika barua hiyo, Waziri wa Mambo ya Ndani ameelezea kujiuzulu kwake ni kwa "maslahi ya taifa" na ya chama, na "kumpunguzia Rais Ramaposa mzigo wa shinikizo uliokuwa ukimkabili".

Taarifa kutoka ofisi ya rais ilisema Bw Gigaba ni miongoni mwa viongozi waandamizi wa chama tawala African Natuional Congress-ANC , kujivua nafasi zao kwa heshima ya nchi yake na harakati zinazomhusu.

Gigaba ana umri wa miaka arobaini na saba , miaka ya hivi karibuni amejikuta katika mkanganyo wa mambo kutokana na kutumia madaraka yake vibaya katika huduma mbalimbali na kuisaidia familia ya wafanyabiashara ya Gupta yenye utata.

Wafanya biashara hao wenye asili ya nchini India wanahusishwa sana na kashfa kadhaa za rushwa chini ya utawala wa Rais Jacob Zuma.katika kila hali ikiwa ni pamoja na Bwana Gigaba, wamekana makosa yoyote.

Malusi Gigaba aliingia matatani mwezi Oktoba baada ya mratibu wa kitaifa, Busisiwe Mkhwebane, kumuomba Rais Cyril Ramaphosa kuchukua "vikwazo" dhidi ya waziri huyo, "kwa kudanganya alipokuwa akila kiapo mbele ya mahakama".

Alikuwa amekataa kujiuzulu mapema mwezi Novemba, akidai kuwa alitaarifuvikosi vya usalama na idara ya ujasusi kuhusu suala hilo.