PPRD na washirika wake waendelea kuonyesha umoja wao DRC
Imechapishwa:
Muungano wa vyama madarakani FCC nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo umeendelea kujiimarisha, huku upinzani ukionekana kugawanyika, wakati umesalia mwezi mmoja na nusu kabla ya Uchaguzi Mkuu nchini humo.
Hata hivyo aanasiasa wa upinzani nchini DRC Jean-Pierre Bemba, Moise Katumbi, Adolphe Muzito na Martin Fayulu wametamatisha mkutano wao wa siku ya Alhamisi Novemba 15 huko Brussels, baada ya Felix Tshisekedi na Vital Kamerhe kujiondoa kwenye mkataba wa Geneva kuhusu uteuzi wa mgombea mmoja wa upinzani
Kubwa katika Mkutano huo ni kwamba wanasiasa hao wa upinzani, wameonyesha uungwaji wao mkono kwa mgombea wa upinzani Martin Fayulu, aliyeteuliwa Jumapili Novemba 11 kupeperusha bendera ya upinzani.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jijini Kinshasa mkurugenzi wa ofisi ya rais Nehemie Mwilanya amesema DRCongo inahitaji kuwapata wanasiasa wazalendo, wenye kuijali nchi yao wasiotaka kutumiwa na watu kutoka nje.
Uchaguzi nchini DRC umepangwa kufanyika tarehe 23 Desemba 2018.