DRC-SIASA

Emmanuel Shadary anadi sera yake katika kapmeni za kisiasa DRC

Mgombea wa chama tawala DRC, Emmanuel Ramazani Shadary, anadi mpango wake kwa uchaguzi wa urais wa Desemba 23, Kinshasa, Novemba 19, 2018.
Mgombea wa chama tawala DRC, Emmanuel Ramazani Shadary, anadi mpango wake kwa uchaguzi wa urais wa Desemba 23, Kinshasa, Novemba 19, 2018. REUTERS/Kenny Katombe

Mgombea wa muungano wa vyama vinavyoshiriki serikalini nchini DRC (FCC) Emmanuel Ramazani Shadary hatimaye amenadi mpango wake, iwapo atafanikiwa kuchaguliwa kama rais wa nchi hiyo. Itahitaji dola bilioni 86 ili kutekeleza mpamgo huo kwa muda wa miaka mitano. Ameahidi kuimarisha mamlaka ya nchi.

Matangazo ya kibiashara

Ni mpango kabambe ambao Emmanuel Ramazani Shadary alizungumzia kwa zaidi ya saa mbili. Mpango huo ni sawa na dola bilioni 86 katika kipindi cha miaka mitano, dhidi dola bilioni 5 ya bajeti ya nchi hiyo mnamo mwaka 2018. Mpango huo unajumuisha mambo manne: "Kuimarisha mamlaka ya nchi na kuboresha utawala wa umma, kuimariha uchumi katika nyanja mbalimbali na ushindani, mapambano dhidi ya umaskini na kuweka sawa mambo mablimbali ya nchi yetu, DRC, "amesema Emmanuel Ramazani Shadary.

Mgombea wa FCC amehadi hasa kutoa ajira 100,000 kufikia mwaka 2020, kuboresha masuala ya upatikanaji wa maji, umeme, mishahara bora kwa walimu na maafisa wa usalama na ugawaji bora wa rasilimali kubwa za taifa. Katika kupambana dhidi ya "ufisadi" na rushwa: "Nitahakikisha kuwa sheria inafanya kazi, ikiwa ni pamoja na matumizi mabaya ya madaraka, kutoadhibu wahalifu, rushwa, ufisadi unaofanywa katika ngazi zote , nitahakikisha vinashughulikiwa kwa mujibu wa sheria za Jamhuri ".

Emmanuel Ramazani pia amempongeza Rais Joseph Kabila ambaye amemtaja kama "mbunifu wa demokrasia ya DRCongo" na ameahidi kuendeleza sera hiyo ikiwa "atachaguliwa kama rais."