ABBA-CPJ-UHURU-WANAHABARI

Mwanahabari wa RFI Hausa Ahmed Abba atuzwa New York

Mwanahabari wa RFI Hausa Ahmed Abba, (Kulia) akipata tuzo kutoka kwa Mkuu wa CPJ Novemba 20 2018 jijini New York nchini Marekani
Mwanahabari wa RFI Hausa Ahmed Abba, (Kulia) akipata tuzo kutoka kwa Mkuu wa CPJ Novemba 20 2018 jijini New York nchini Marekani https://cpj.org/

Mwanahabari wa RFI Hausa Ahmed Abba, hatimaye amepata tuzo ya mwaka 2017 kutoka Kamati maalum ya kuwalinda Wanahabari CPJ, katika hafla iliyofanyika siku ya Jumanne jijini New York nchini Marekani.

Matangazo ya kibiashara

Abba mwenye umri wa miaka 38 raia wa Cameroon, alipata tuzo hiyo baada ya kukamatwa mwezi Julai mwaka 2015, baada ya kwenda kuripoti kuhusu uvamizi wa kundi la kigaidi la Boko Haram Kaskazini mwa Cameroon.

Baada ya kuzuiwa jela kwa muda wa miezi 29, kwa madai ya kushirikiana na Boko Haram ambayo yalibainika kuwa sio kweli, Abba, aliachiliwa huru mwezi Desemba mwaka 2017, kutokana na shinikizo kutoka kwa wanaharakati wa kutetea Wanahabari na wale wa  binadamu.

Abba pia alishudhuria tuzo za 28 zilizotolewa kwa Wanahabari watano wanawake ambao wamekuwa katika harakati kubwa za kuleta mabadiliko katika nchi zao, licha ya kupigwa na polisi na hata kufungwa jela, kwa lengo la kutetea haki za wanyonge.

Wanawake watano waliotuzwa na Kamati maalum ya Wanahabari CPJ jijini New York Novemba 20 2018
Wanawake watano waliotuzwa na Kamati maalum ya Wanahabari CPJ jijini New York Novemba 20 2018 https://cpj.org/

Miongoni mwa Wanahabari hao ni Amal Khalifa Idris Habbani, kutoka Sudan, Nguyen Ngoc Nhu Quynh kutoka Vietnam.

Wengine ni Luz Mely Reyes kutoka Venezuela na Anastasiya "Nastya" Stanko kutoka Ukraine.

Kamati ya CPJ ni miongoni mwa mashirika ya Kimataifa yanayotetea haki za wanahabari duniani na kushinikiza serikali, kuwalinda na kuruhusu uhuru wa vyombo vya Habari.