CAR-MINUSCA-USALAMA

Minusca mashakani baada ya mauaji ya Alindao, Jamhuri ya Afrika ya Kati

Uwepo wa Walinda amani wa Minusca katika mji wa Alindao haukuzuia vifo vya watu zaidi ya 60 Novemba 15, 2018.
Uwepo wa Walinda amani wa Minusca katika mji wa Alindao haukuzuia vifo vya watu zaidi ya 60 Novemba 15, 2018. AFP/Florent Vergnes

Serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati imetangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa baada ya shambulio katika kambi ya wakimbizi ya Alindao Novemba 15, ambapo watu zaidi ya 60 waliuawa, kwa mujibu wa ripoti ya hivi karibuni ya shirika la Habari la AFP.

Matangazo ya kibiashara

Timu kadhaa zilikwenda siki ya Jumatano wiki hii katika eneo la tukio ili kujaribu kujua hali halisi na mambo yanayohitajika. Ikiwa idadi ya watu waliouawa bado haijajulikana, mazingira ya tukio hilo pia hayajulikani na hali hiyo imeibua maswali mengi, ikiwa ni pamoja na maswali kuhusu hatua ya Minsuca.

Wengi wanajiuliza jinsi gani tukio hilo liliweza kutokea mbele ya macho ya kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati (Minusca). Msemaji wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo, Vladimir Monteiro, amesema mapigano hayo hayakuwa yametarajiwa na idadi ya kikosi cha Umoja wa Matiafa kilikuwa hakitoshi kwa kuzima shambulio hilo.

"Hakukua na idadi ya kutosha ya askari, lakini askari wetu waliingilia kati, msemaji wa Minusca amesema. Kambi moja ya Minusca ina askari 50. Na kambi kama hiyo ndio tunayo katika mji wa Alindao. Leo, tumeimarisha kikosi chetu, tumetuma askari wengine kutoka Bambari na eneo jingine ili kuimarisha ngome yetu, kuendelea kupiga doria nakuzuia mapigano mapya. "

Viongozi wawili wa kidini ni miongoni mwa waathirika wa Alindao. Baadhi ya watu waliouawa, wengi walichomwa moto na wengine walikatwa katwa.

"Picha tulizoona, zinaonyesha uhalifu dhidi ya ubinadamu uliofanywa, " amesema Askofu mkuu wa Bangui.

Askofu mkuu wa Bangui ameaomba utulivu na kuepuka kuingia kwenye mtego wa mgogoro wa kidini.