ICC-HAGUE-BANGUI-SELEKA-ANTI-BALAKA

Mshukiwa wa mauaji nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati kufikishwa ICC

Majaji wa Mahakama ya Kimataifa ya ICC mjini Hague nchini Uholanzi
Majaji wa Mahakama ya Kimataifa ya ICC mjini Hague nchini Uholanzi REUTERS/Toussaint Kluiters

Kiongozi wa zamani wa kundi la waasi nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati Alfred Yekatom, atafikishwa kwa mara ya kwanza mbele ya Majaji wa Mahakama ya Kimataifa ya ICC, kufunguliwa mashtaka ya uhalifu wa kivita siku ya Ijumaa.

Matangazo ya kibiashara

Mshukiwa huyo ambaye jina lake maarufu ni "Colonel Rambo alikamatwa mwezi uliopita na kusafirishwa jijini Hague nchini Uholanzi baada ya kutolewa agizo la kutafutwa.

Yekatom mwenye umri wa miaka 43, anakabliwa na mashtaka 14 ,yaliyosababisha mapigano makali kati ya waasi wa Kikiristo na Waislam nchini mwake tangu mwaka 2013 na kusababisha maelfu ya raia wa kawaida kupoteza maisha na wengine kuyakimbia makwao.

Hadi kukamatwa kwake, alikuwa ni mbunge na alikamatwa katika majengo ya bunge jijini Bangui, na katika harakati za kumtia mbarani, alifwatua risasi hewani lakini akalamewa na maafisa wa usalama.

Majaji, wanatarajiwa kumtambua mshukiwa huyo na kumsomea mashtaka ya mauaji, mateso, kuwaajiri watoto katika jeshi lake, miongoni mwa mashtaka mengine yanayomkabili.