UFARANSA-AFRIKA-SANAA

Ufaransa kurejesha kazi za sanaa barani Afrika

Serikali ya Ufaransa inabadilisha sheria, ili kazi za sanaa zilizofanywa na Waafrika,  kipindi cha ukoloni, zirejeshwe katika nchi zao.

Kazi mojawpao ya sanna kutoka barani Afrika iliyohifadhiwa nchini Ufaransa
Kazi mojawpao ya sanna kutoka barani Afrika iliyohifadhiwa nchini Ufaransa dapper.fr
Matangazo ya kibiashara

Ahadi hii ilitolewa na rais Emmanuel Macron, mwaka mmoja uliopita, baada ya kutembelea Burkina Faso, na kuahidi kuwa kazi hizo za sanaa, zitarejeshwa barani Afrika.

Sheria hii mpya, inaeleza kuwa kazi zote za sanaa, zilizo katika makavazi ya serikali, zilizotengenezwa wakati wa ukoloni, sio za Ufaransa kwa sababu, zilipelekwa nchini humo, bila ya ruhusa kutoka kwa wenyeji.

Miongoni mwa kazi hizo za sanaa, ni pamoja na michongo ya watu mashuhuri, wanyama na vitu vingine mbalimbali vinavyoelezea historia.

Wachambuzi wa mambo wanasema hatua hii ya Ufaransa huenda ikaishinikiza Uingereza ambayo ilikuwa koloni ya nchi kadhaa barani Afrika, kurejesha kazi hizo saa katika koloni zao za zamani.