DRC-SIASA-UPINZANI-UCHAGUZI

Felix Tshisekedi kupeperusha bendera ya upinzani kando na Fayulu

Viongozi wawili wa upinzani Vital Kamerhe (kushoto) na Félix Tshisekedi (kulia) wakitangaza kuungana jijini  Nairobi,  23 Novemba 2018.
Viongozi wawili wa upinzani Vital Kamerhe (kushoto) na Félix Tshisekedi (kulia) wakitangaza kuungana jijini Nairobi, 23 Novemba 2018. AFP/Yasuyoshi Chiba

Mgombea wa upinzani katika uchaguzi muhimu wa rais unaopangwa kufanyika Disemba 23 nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo Felix Tchisekedi, anaingia katika kinyanganyiro hicho akiwa na ushawishi wa kisiasa kama mwana wa Marehemu Etienne Tshisekedi, mwanzilishi wa chama cha UDPS

Matangazo ya kibiashara

Felix Tshisekedi na Vital Kamerhe ambao walioondoa saini zao katika makubaliano ya Geneva Uswis kuhusu upinzani kuwa na mgombea mmoja ambaye ni Martin Fayulu hapo jana wamekubaliana kuwa Felix ndiye atakayepeperusha bendera ya upinzani.

Hii ina maana kwamba upinzani utakuwa na wagombea wawili ambao ni Martin Fayulu, na Felix Tshisekedi ambao watapambana na mgombea wa muungano wa vyama vinavyomuunga mkono rais Kabila FCC katika Uchaguzi Mkuu wa tarehe 23 mwezi Desemba, Mwaka huu.

Viongozi Hawa wawili wa upinzani Felix Tshisekedi wa UDPS na Vital Kamerhe wa UNC wamefikia makubaliana hayo katika mkutano unaofanyika katika hoteli serena ya jijini Nairobi nchini Kenya, ambako waliwasili usiku wa kuamkia leo.

Katika hatua nyingine baraza la maaskofu wa kanisa katoliki wameendelea kuonyesha mashaka kuhusu suala la matumizi ya mashine za kupigia kura ameeleza Donantien Nshole, katibu mkuu wa CENCO
 

Kwa upande wa Alain Atundu ambaye ni msemaji wa upande wa chama tawala amesisitiza kuwa uchaguzi utakao fanyika utakuwa huru na haki.