Marekani yasema, magaidi wanapanga kushambulia taasisi zake nchini DRC
Imechapishwa:
Ubalozi wa Marekani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, unasema upokea taarifa za uwezekano wa kutokea kwa shambulizi la kigaidi jijini Kinshasa kulenga taasisi zake.
Onyo hili limekuja, wiki nne kuelekea Uchaguzi wa kihistoria nchini humo. Ubalozi huo unasema taarifa hizo ni sahihi na zimethibitishwa.
Siku ya Jumatatu, ubalozi huo utafungwa na raia hatawataruhusiwa kuingia kwa sababu za kiusalama.
“Ubalozi wa Marekani jijini Kinshasa umepokea taarifa za uhakika kuwa, kuna uwezekano wa kutokea kwa shambulizi, kulenga taasisi za Marekani jijini Kinshasa,” taarifa hiyo imeandikwa kwenye tovuti yake.
Raia wa Marekani wanaoishi nchini DRC wametakuwa kuwa makini.
“Raia wa Marekani wanaoishi nchini DRC, wanatakiwa kuwa macho, na kuripoti kisa chochote ambacho kinaashiria hatari dhidi yao,” taarifa huyo iliendelea kueleza.
Eneo la Mashariki, limeendelea kushuhudia usalama mdogo, kutokana na kuwepo kwa makundi ya waasi kama ADF NALU, yanayoendelea kuwavamia raia wa serikali, hasa Wilayani Beni, eneo ambalo linakabiliwa na ugonjwa hatari wa Ebola.