UGANDA-EBOLA-WHO-DRC

Maambukizi ya Ebola yaongezeka mjini Butembo nchini DRC

Watalaam wa ugonjwa wa Ebola
Watalaam wa ugonjwa wa Ebola ®MSF

Idadi ya waathirika wa ugonjwa wa Ebola nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo imeendelea kuongezeka katika Wilaya ya Butembo na maeneo mengine licha ya kupungua katika wilaya ya Beni.

Matangazo ya kibiashara

Ripoti ya wizara ya afya nchini humo, inaeleza kuwa, katika kipindi cha wiki ijayo, watu 10 wamepoteza maisha.

Zaidi ya asilimia ya wanawake sitini wamefariki dunia kutokana na ugonjwa huu, wanawake Ishirini na sita huko Butembo wamefariki na watoto 12,” amesema Jean Christoph, kiongozi wa wauguzi wa Ebola mjini Butembo.

Nalo Shirika linalowahudumia watoto duniani UNICEF, limesema watoto kadhaa wamesalia mayatima, baada ya wazazi wao kupoteza maisha.

“Kuna watoto piya ambao wamebaki kuwa mayatima ,baada ya wazazi wao kufariki na Ebola lakini shirika la UNICEF lajihusisha na watoto hao piya jamaa zao,” amesema Guido Carnal Mkuu wa UNICEF.

Serikali ya mji wa Butembo, imewataka raia kuendelea kuchukua tahadhari, kuhusu maambukizi ya Ebola.

Watu zaidi ya 200 wamepoteza maisha, katika Jimbo la Kivu Kaskazini tangu mwezi Agosti kwa mujibu wa takwimu za Shirika la afya duniani WHO.