GAMBIA-HAKI
Gambia yaruhusu raia wake kuwasilisha kesi zao katika mahakama ya Afrika
Imechapishwa:
Jamuhuri ya Gambia imekuwa nchi ya tisa kuruhusu taasisi zisizokuwa za kiserikali na raia wake kuwasilisha kesi katika mahakama ya Afrika yenye makao yake makuu jijini Arusha nchini Tanzania.
Matangazo ya kibiashara
Kwa mujibu wa msajili wa mahakama hiyo ya Afrika Dokta Robert Eno,Gambia imeridhia raia wake kufikisha kesi katika mahakama hiyo moj akwa moja.
Hatua hiyo ilifikiwa baada ya rais Adama Barrow kutia sahihi mnamo Octoba 23 mwaka huu.
Mataifa mengine yalikwishaunga mkono mahakama hiyo ni Benin Burkina faso,Cote d'Ivoire Ghana Malawi Mali na Tanzania.