DRC-MAREKANi-USALAMA

Marekani yafunga ubalozi wake kufuatia hali ya usalama DRC

Askari wa FARDC wakipiga doria karibu na makao makuu ya Radio na Televisheni ya serikali (RTNC) Kinshasa tarehe 30 Desemba 2013.
Askari wa FARDC wakipiga doria karibu na makao makuu ya Radio na Televisheni ya serikali (RTNC) Kinshasa tarehe 30 Desemba 2013. © AFP

Ubalozi wa Marekani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, unafungwa tangu Jumatatu wiki hii baada ya kutoa taarifa ya uwezekano wa kutokea kwa mashambulizi yanayolenga taasisi zake.

Matangazo ya kibiashara

Uamuzi huu wa Marekani imekuja, wiki nne kuelekea Uchaguzi wa kihistoria nchini humo.

Ubalozi huo umewataka raia wake nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kuchukua tahadhari.

Hayo yanajiri wakati Askofu Mkuu mpya wa Kanisa Katoliki, Fridolin Ambongo, ametoa wito wa uvumilivu kwa raia wa nchi hiyo kuelekea Uchaguzi Mkuu tarehe 23 mwezi ujao.

Nalo Baraza la Maaskofu wa Kanisa hilo CENCO, limetoa wito wa kufanyika kwa Uchaguzi, utakaoaminika na kuwa huru na haki.