NIGERIA-BOKO HARAM-USALAMA

Vikosi vya usalama na ulinzi vyaendelea kulengwa katika mashambulizi ya Boko Haram Nigeria

Katika wiki za karibuni, jeshi la Nigeria limeendelea kuimarisha ngome zake kaskazini-mashariki mwa nchi, ikiwa ni pamoja na Maiduguri.
Katika wiki za karibuni, jeshi la Nigeria limeendelea kuimarisha ngome zake kaskazini-mashariki mwa nchi, ikiwa ni pamoja na Maiduguri. AFP

Mamluki kutoka Afrika Kusini alikuwa katika mstari wa mbele kupambana na magaidi wa Boko Haram nchini Nigeria, amemshtumu rais Muhammadu Buhari kwa uamuzi mbaya wa kisiasa katka vita dhidi ya kundi hilo.

Matangazo ya kibiashara

Kupitia ukurasa wake wa facebook, Eeben Barlow ameshtumu rais Buhari kwa kusema kuwa, kwa kisiasi kikubwa Boko Haram wameshindwa, licha ya kundi hilo kuendelea kutekeleza mashambulizi zaidi ya kigaidi, kuwauwa wanajeshi na kuchukua silaha.

Ukosoaji huu unakuja, baada ua ripoti kuwa wanajeshi wa Nigeria zaidi ya 100 waliuawa baada ya kushambuliwa na wanagambo wa Boko Haram, hivi karibuni, madai ambayo jeshi linakanusha.

Nigeria na nchi jirani zimeendelea kukumbwa na mashambulizi ya kundi la Boko Haram, ambalo limeuwa mamia ya watu na kuwateka mamia wengine.