DRC-UN-UCHUNGUZI

DRC yakerwa na uchunguzi kuhusu mauaji ya wataalam wa Umoja wa Mataifa

Kuvuja kwa maelfu ya kurasa za nyaraka za siri za Umoja wa Mataifa kunatoa mwanga mpya kuhusu mauaji ya wataalam wa Umoja huo Michael Sharp na Zaida Catalan.
Kuvuja kwa maelfu ya kurasa za nyaraka za siri za Umoja wa Mataifa kunatoa mwanga mpya kuhusu mauaji ya wataalam wa Umoja huo Michael Sharp na Zaida Catalan. © RFI

Maelfu ya kurasa za nyaraka za siri za Umoja wa Mataifa zinazohusiana na mauaji ya wataalam wawili walioagizwa na Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa zimevuja. Michael Sharp na Zaida Catalan walipewa kazi ya kuchunguza kuhusu machafuko nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Matangazo ya kibiashara

"Congo Files" inachunguza njia na mambo yaliyotolewa na wachunguzi pamoja na matatizo waliokabiliana nayo kati ya mwezi Machi 2017 na mwezi Septemba 2018. kazi yao ilitokana na ushirikiano kati ya vyombo vya habari kadhaa vya kimataifa: RFI, Le Monde, Foreign Policy, Süddeutsche Zeitung na televisheni ya Sweden. Nyaraka hizi zinafichua uchunguzi wa kina wa maafisa wa polisi wa Umoja wa Mataifa na utaratibu wanaoutumia katika kutafuta ukweli. Sehemu mbili za kwanza za uchunguzi huu ni ushirikiano kati ya wachunguzi hao na Sonia Rolley (RFI) pamoja na Joan Tilouine (Le Monde).

Ni video inayotisha. Inachukua dakika sita na sekunde kumi na saba. Lakini inaonekana kutokuwa na mwisho kwa waandishi hawa wa habari walioitishwa na mamlaka kutazama video hiyo katika mji wa Kinshasa Jumatatu, April 24, 2017. Hata hivyo saa chache baadae video hiyo ya mauaji ya wataalamu wawili wa Umoja wa Mataifa ilizunguka dunia nzima kupitia mitandao ya kijamii. video hiyo inaonesha vijana wenye silaha wakivalia kichwani vitambaa vyenye rangi nyekundu wakiwapiga risasi wataalam hao.

Tukio hilo lilitokea katika bonde la Bunkonde, kijiji kinachozungukwa na makaburi ya halaiki, katikati mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC). Wataalam hao waliouawa ni Michael Sharp, raia wa Marekani mwenye umri wa miaka 34 na Zaida Catalan, raia wa Sweden mwenye umri wa miaka 36, madereva wao watatu na mkalimani wao, raia wa DRC. Wataalam hao walikuwa wakichunguza kwa niaba ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu uhalifu uliokuwa unaendelea katika mikoa ya Kasai. Miezi saba kabla ya mauaji hayo, kiongozi wa kijadi Kamuina Nsapu, ambaye alikuwa aliasi dhidi ya serikali ya DRC, aliuawa na jeshi. Wafuasi wake, baadaye waligeuka na kuwa wanamgambo wa kisiasa huku wakikabiliana na vikosi vya usalama na ulinzi.

Kwa upande wa serikali ya DRC, wafuasi hawa wa Kamuina Nsapu ni"magaidi".

Serikali ya DRC inashtumu wafuasi hao wa Kamuina Nsapu kwamba ndio walihusika na maauji ya wataalamu wawili wa Umoja aw Mataifa, Michael Sharp na Zaida Catalan.