GABON-SIASA-AFYA

Sylvia Bongo: Ali Bongo ataondoka Riyadh Jumatano kuelekea Rabat

Rais wa Gabon Ali Bongo katika mkutano wa 10 wa Brics Julai 27 huko Johannesburg.
Rais wa Gabon Ali Bongo katika mkutano wa 10 wa Brics Julai 27 huko Johannesburg. MIKE HUTCHINGS / POOL / AFP

Rais wa Gabon Ali Bongo Ondimba, ambaye amekuwa hospitali tangu Oktoba 24 katika mji mkuu wa Saudi Arabia, Riyadh, anatarajia kuondoka Jumatano kwenda Rabat, mkewe wake Sylvia Bongo Ondimba ametangaza.

Matangazo ya kibiashara

"Jumatano, Novemba 28 (...), Ali Bongo Ondimba, mume wangu, ataondoka hospitali ya King Faisal mjini Riyadh, nchini Saudi Arabia," ameandika Bongo, akiongeza kuwa atawasili siku hiyo hiyo katika "mji wa Rabat", nchini Morocco .

Bi Bongo Ondimba amesema yeye na mumewe "wanataka kutoa" "shukrani zao za dhati kwa mamlaka ya Saudi Arabia na matabibu waliomshughulikia alipokuwa amelazwa hospitalini".

"Kwa kuendelea na mapumziko, rais, baada ya kushauriana na familia yake ya karibu, ameamua kukubali ombi la ndugu yake, Mfalme wa Morocco Mohammed wa 6 kupumzika kwa siku kadhaa mjini Rabat kabla ya kurejea nchini Gabon. Tunashukuru sana," amesema Sylvia Bongo.

Amesema kuwa kuruhusiwa kuondoka Riyadh kwenda Rabat "kulitokana na jinsi hali ya afya ya mumewe inavyoendelea.

Rais Bongo anatarajia "kuchukua muda wa kutosha wa kupumzikakabla ya kuendelea na majukumu yake pamoja na masuala mbambali yanayopewa kipaumbele yanayomsubiri nchini Gabon" , kwa mujibu wa mkewe.

"Kufuatia hatua hiyo, rais amewataka maafisa wakuu katika ofisi ya rais nchini Gabon kufanya safari kwenda kukutana naye mjini Rabat," Bi Bongo amesema.

Rais wa Gabon na Mfalme Mohammed wa 6 wa Morocco wana uhusiano wa karibu tangu utoto wao.