CAMEROON-NIGERIA-BOKO HARAM

Watu 29 wajeruhiwa katika shambulizi la kigaidi Kaskazini mwa Cameroon

Kiongozi wa Boko Harama Abubakar Shekau
Kiongozi wa Boko Harama Abubakar Shekau © AFP PHOTO / BOKO HARAM

Watu 29 wamejeruhiwa Kaskazini mwa Cameroon, baada ya kutokea kwa shambulizi la bomu la kujitoa mhanga, katika eneo ambalo limekuwa likishambuliwa mara kwa mara na kundi la kigaidi la Boko Haram.

Matangazo ya kibiashara

Walioshuhudia na kuponea shambulizi hilo, wanasema, mlipuaji huyo ambaye anaaminika kuwa alikuwa mwanamke, alijilipua  siku ya Jumatano asubuhi katika mji wa Amchide mpaka na Nigeria.

Kwa muda wa karibu miaka mitatu sasa, Camerooon imekabiliwa na mashambulizi ya Boko Haram Kaskazini mwa nchi hiyo.

Mashambulizi hayo yamesababisha vifo vya zaidi ya watu 1,500 na kusababisha wengine zaidi ya 155,000 kukimbia makwao.

Kundi la Boko Haram kutoka Nigeria, limekuwa likitekeleza mashambulizi katika nchi jirani ya Cameroon kuanzia mwaka 2011.

Mbali na ugaidi, Cameroon pia inakabiliwa na mzozo wa kisiasa na usalama katika maeneo yanayozungumza lugha ya Kiingereza, kutaka kuunda nchi yao.