NIGERIA-BOKO HARAM-USALAMA

Buhari aahidi kwa mara nyingine kuangamiza Boko Haram

Le président nigérian Muhammadu Buhari aux Nations unies à New York le 28 septembre 2018.
Le président nigérian Muhammadu Buhari aux Nations unies à New York le 28 septembre 2018. REUTERS/Darren Ornitz/File Photo

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari amefanya ziara ya kikazi ya siku moja katika mji wa Maiduguri, mji mkuu wa jimbo la Borno ambako limezaliwa kundi la wanamgambo wa kiislamu la Boko Haram.

Matangazo ya kibiashara

"Kundi la Boko Haram linapaswa kuangamizwa duniani," Rais Muhammadu Buhari alisema Jumatano (Novemba 28), wiki moja baada ya shambulio dhidi ya kambi ya jeshi. Shambulio ambalo liliuawa mamia ya watu ikiwa ni pamoja na wanajeshi.

Rais wa Nigeria alikuwa akizungumza katika mkutano wa kila mwaka wa viongozi wakuu wa kijeshi huko Maiduguri, katika Jimbo la Borno, miezi michache kabla ya uchaguzi wa uraisuliopangwa kufanyika mwezi Februari 2019.

Miezi mitatu kabla ya uchaguzi wa urais, Rais Buhari ameanzisha tena vita vyake dhidi ya Boko Haram. Rais Buhari anakabiliwa na shinikizo kubwa. Alipochukua hatamu ya uongozi wa nchi mwezi Machi 2015, aliahidi kutokomeza kuni la wanamgambo wa Kiislamu la Boko Haram , lakini katika miezi ya hivi karibuni mashambulizi ya kundi hilo yameongezeka kwa kasi.

Mashambulizi yasiopunguwa 17 au majaribio ya mashambulizi dhidi ya kambi za jeshi yameorodheshwa tangu mwezi Julai kwa mujibu wa shirika la Habari la AFP.

Jumatano, Novemba 28, Rais Buhari aliwapongeza askari wake waliokusanyika huko Maiduguri. "Mafanikio makubwa yamefanyika kwa kurejesha usalama kaskazini-mashariki mwa nchi," alisema kabla ya kutoa heshima zake za mwisho kwa askari waliouawa katika mashambulizi ya hivi karibuni. "Ninawahakikishia kuwa serikali hii inafahamu vema mazingira mnayoishi. Ninachoweza tu kufanya ni kuwakuhimiza kuendelea na jukumu lenu kama watetezi wa kwa usalama na amani ya nchi hii. Ndiyo sababu mlikula kiapo na ndiyo maanda mimi napaswa kutekeleza jukumu hilo kama amri mkuu wa majeshi, " Buhari alisema.

Buhari pia aliahidi kufanya kazi na washirika wa kikosi cha pamoja cha kimataifa ambacho majukumbu yake ni kupamfamana dhidi ya makundi ya wanamgambo wa Kiislamu.