DRC-EBOLA-AFYA

Watu waendelea kufariki dunia kufuatia mlipuko wa Ebola mashariki mwa DRC

Timu inayopambana dhidi ya mlipuko wa ugonjwa wa Ebola katika Hospitali ya Bikoro nchini DRC.
Timu inayopambana dhidi ya mlipuko wa ugonjwa wa Ebola katika Hospitali ya Bikoro nchini DRC. REUTERS/Jean Robert N'Kengo

Takribani watu 19 wamefariki dunia katika kipindi cha siku tano mashariki mwa DRC ambako kunashuhudia mlipuko wa ugonjwa wa Ebola,tangu mwezi Agosti, wizara ya afya nchini humo imefahamisha.

Matangazo ya kibiashara

Hadi sasa jumla ya watu 241 wamefariki dunia kama ambavyo serikali ya DRC imethibitisha kupitia wizara ya afya.

Visa vingine 74 vinaendelea kuchunguzwa wakati huu jumla kuu ya visa ikiwa ni 421 miongoni mwao 374 vimethibitishwa lakini 47 bado kuthibitishwa.

Asilimia 60 ya waliofariki kutokana na ugonjwa huu ni wanawake kama ilivyoelezwa juma hili na Jean Christophe, kiongozi wa wauguzi wa Ebola mjini Butembo.

Aidha Shirika linalowahudumia watoto duniani UNICEF, limesema watoto kadhaa wamebaki yatima, baada ya wazazi wao kupoteza maisha.

Serikali ya DRC, imewataka raia kuendelea kuchukua tahadhari, kuhusu maambukizi ya Ebola.