DRC-UCHAGUZI-SIASA

Felix Tshisekedi na Vital kamerhe wazindua kampeni yao Camp Luka

Félix Tshisekedi (upande wa kulia) na Vital Kamerhe (upande wa kushoto) walipofika Kinshasa Novemba 27, 2018 (picha ya kumbukumbu).
Félix Tshisekedi (upande wa kulia) na Vital Kamerhe (upande wa kushoto) walipofika Kinshasa Novemba 27, 2018 (picha ya kumbukumbu). © John WESSELS / AFP

Wanasiasa wawili wa upinzani walioondoa saini zao kwenye makubaliano ya uteuzi wa mgombea mmoja Martin Fayulu, waliendesha kampeni yao ya uchaguzi mjini Kinshasa siku ya Jumapili Desemba 2.

Matangazo ya kibiashara

Felix Tshisekedi na Vital Kamerhe walikutana na wafuasi wao katika moja ya eneo maarufu la Camp Luka mji muu wa DRC.

Ilikuwa suala la kuzindua kampeni ya mgombea Felix Tshisekedi ambaye anawania kwenye kiti cha urais katika Uchaguzi Mkuu uliopangwa kufanyika Desemba 23.

Katika hotuba yao fupi, mbele ya wafuasi wao, Vital Kamerhe na Félix Tshisekedi wameeelezea umaskini unaolikabili ene hilo maarufu katika mji wa Kinshasa na kutoa maneneo makali dhidi ya utawala: "Ni mambo ya kushangaza kabisa na ya aibu, kwa kile tunachoona hapa. Tunapaswa kuwa tukifanya hivyo, tusifanye tu kampeni zetu katika maeneo yaliyoendelea kimiundombinu, Barabara, umeme, maji...). Tunapaswa kuja hapa Camp Luka ili kuona maisha magumu yanayowakabili wananchi wa DRC. "

Mbali na wafuasi wa vyama vya UNC na UDPS, wafuasi kadhaa, hasa vijana wa mwanasiasa wa upinzani na mgombea urais Martin Fayulu pia wamehudhuria katika kameni za wanasiasa hao wawili. Jambo hilo halimkera Vital Kamerhe, kama alivyosema mwenyewe: "Kuna wagombea wengi, na hii ndiyo demokrasia. Sio vibaya, inamaanisha kuwa eneo hili ni ngome ya upinzani. Ni jambo zuri sana. Hakuna upinzani au mgawanyiko kati ya pande mbili za upinzani, watu wanapaswa kujua hivo, sisi sote tunapigana kwa ajili ya mabadiliko ya nchi yetu.

"Camp Luka ni hatua ya kwanza ya kampeni ambayo itaendelea hadi Kinshasa leoJumatatu, Desemba 3 kabla ya kuelekea mashariki mwa nchi.