DRC-UCHAGUZI-SIASA

Kampeni za uchaguzi zapamba moto DRC

Tume ya Kitaifa ya Uchaguzi (CENI) imeonyesha mashine ya kupigia kura itakayotumika katika uchaguzi wa Desemba 23.
Tume ya Kitaifa ya Uchaguzi (CENI) imeonyesha mashine ya kupigia kura itakayotumika katika uchaguzi wa Desemba 23. © AFP

Kampeni za uchaguzi zinaendelea kushika kasi nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo ikiwa zimesalia wiki tatu kabla ya Uchaguzi Mkuu uliopangwa kufanyika Desemba 23.

Matangazo ya kibiashara

Mgombea wa chama tawala Emmanuel Ramazani Shadary anatarajia kujielekeza Magharibi mwa nchi hiyo baada ya kufanya kampeni zake mashariki mwa nchi hiyo, huku Upinzani nao ukipanga kuaanza kampeni zake mashariki mwa nchi

Aidha wagombea wengi wa kiti cha urais wanaendelea kujiuzulu na kuwaunga mkono wagombea wa Upinzani Felix Tchisekedi na martin Fayulu.

Jean Philibert Mabaya mgombea kiti cha urais kwa tiketi ya chama cha Arc en Ciel ametangaza kujiunga na muungano Lamuka na amewatolea wito wagombea wanaowania kiti cha ubunge kwa niaba ya chama chake kumpigia debe Martin Fayulu.

Wakati huo huo huko muungano wa FatshiVit chini ya mgombea Felix Tshisekedi alieungana na Vital Kamerhe umewapokea Kin Key Mulumba, Charles Bofassa Djema waliondoka katika muungano kwa ajili ya jamuhuru chini ya Adolphe Muzito na Augustin Kibasa Maliba ambao wataendesha kampeni katika mikoa ya Bandundu, Equateur na Katanga.

Wagombea hao wanatarajiwa kupishana mashariki mwa DRCongo ambapo Jumanne waiki hii muungano unaongozwa na Felix Tshisekedi na Vital Kamerehe unatarajiwa kutuamjini Goma, baadae Bukavu na Uvira.