DRC-SIASA

Joseph Kabila kuwania kiti cha urais mwaka wa 2023

Rais wa DRC, Joseph Kabila, Septemba 2018 Kinshasa.
Rais wa DRC, Joseph Kabila, Septemba 2018 Kinshasa. © JOHN WESSELS / AFP

Rais Joseph Kabila anaye maliza muda wake nchini DRC ametoa hoja ya kuendelea na siasa nchini humo licha ya kuwa hatowania kwa muhula wa pili katika uchaguzi wa urais uliopangwa kufanyika Desemba 23.

Matangazo ya kibiashara

Rais Kabila Kabange hajafutilia mbali uwezekano wake wa kuwania tena urais katika uchaguzi mkuu mwingine utakaofayika mnamo mwaka 2023.

Katika mahojiano na vyombo vya habari vya Marekani Desemba 9, 2018, Rais Kabila amesema kuna uwezekano arudi na kuwania katika uchaguzi wa urasi wa 2023, miaka mitano baada ya uchaguzi wa urais wa Desemba 23.

"Kwa nini kusubiri mpaka mwaka 2023 ili kuendelea na hali ya mambo? amehoji rais Joseph Kabila katika mahojiano na vyombo vya habari nane vya kimataifa. Katika maisha kama siasa, sitarajii kuondoka".

Mwezi Agosti, Bw Kabila alimtangaza mshirika wake wa karibu Emmanuel Ramazani Shadary ambaye ni waziri wa zamani wa mambo ya ndani kuwa mgombea wa muungano wa kisiasa unaotawala kwa sasa.

Bw Shadary amewekewa vikwazo na Umoja wa Ulaya kutokana na tuhuma za ukiukaji wa haki za kibinadamu.

Kumekuwa na wasiwasi kutoka kwa upinzani na jamii ya kimataifa kuhusu iwapo uchaguzi wa DRC utakuwa huru na wa haki.