DRC-EBOLA-AFYA

Watoto wengi waambukizwa virusi vya Ebola DRC

Kitengo kinachohusika na kuwaondoa wagonjwa wa Ebola katika makazi ya watu, DRC wakati wa mlipuko wa virusi vya Ebola mwaka 2009.
Kitengo kinachohusika na kuwaondoa wagonjwa wa Ebola katika makazi ya watu, DRC wakati wa mlipuko wa virusi vya Ebola mwaka 2009. Luis Encinas/MSF

Umoja wa Mataifa unasema kuwa karibu robo tatu ya watu walioambukizwa virusi vya ugonjwa wa Ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ni watoto, huku mamia kati yao wakiwa ama ni yatima au kutengwa na familia zao.

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa shirika la afya duniani WHO jumla ya watu 300 wameshapoteza maisha tangu ugonjwa huo ulipozuka mwezi Agosti mwaka huu huku visa vingi vikiripotiwa kwenye mji wa Beni.

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia watoto UNICEF linasema kuwa kwa kushirikiana na mashirika mengine ya kiraia wamebaini watoto zaidi ya 400 ambao wamekuwa yatima au kutengwa na familia zao tangu kuzuka kwa ugonjwa huo.

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo inaendelea kukabiliwa na ugonjwa wa Ebola, ambao kwa mara ya kwanza umeripotiwa nchini humo mwaka 1976.