MALI-AMNESTY INTERNATIONAL-HAKI

Amnesty International yaomba Mali kufanyia marekebisho sheria ya maridhiano ya kitaifa

Mpiganaji wa kundi la waasi la Azawad karibu na mji wa Kidal, Mali, Septemba 28, 2016.
Mpiganaji wa kundi la waasi la Azawad karibu na mji wa Kidal, Mali, Septemba 28, 2016. © AFP

Shirika la kimataifa la Haki za binadamu la Amnesty International limeiomba serikali ya Mali kufanya marekebisho ya sheria mpya ambayo inatarajiwa kujadiliwa Alhamisi wiki hii katika bunge la nchi hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa vyanzo kutoka shirika hilo sheria hiyo inaweza kuruhusu watu ambao wamehusika katika mauaji, mateso na majanga mengine kukwepa sheria.

"Inahofiwa kuwa polisi kadhaa ambao wanahusika kwa ukiukwaji wa haki za binadamu na watu kutoka makundi ya waasi ambao walihusika katika ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu hawawezi kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria kama muswada huo wa sheria utapitishwa," Samira Daoud, Naibu Mkurugenzi wa kikanda wa Amnesty International Afrika Magharibi na Kati amesema.

"Muswada huu wa sheria utawapa nafasi watu waliojiunga na makundi ya waasi ambao hawakuhusika na mauaji, kutofuatiliwa na vyombo vya sheria, ", alisema Rais wa Mali Ibrahim Boubacar Keita tarehe 31 Desemba 2017. Lakini kwa mujibu wa Amnesty International, muswada huo wa sheria una vipengele vilivyoandikwa "kwa maneno yasiyoeleweka."