DRC-SIASA-UCHAGUZI

Ghala la CENI wilayani Beni Mashariki mwa DRC lavamiwa

Mashine ya kupigia kura itakayotumika katika uchaguzi wa Desemba 23 nchini DRC
Mashine ya kupigia kura itakayotumika katika uchaguzi wa Desemba 23 nchini DRC © AFP

Mamlaka nchini DRC imesema ghala la tume ya uchaguzi wilayani Beni mashariki mwa DRC limevamiwa na waasi jumapili juma moja kabla ya uchaguzi uliopangwa kufanyika nchini DRC ambako mamlaka inajiandaa kufunga mipaka yake.

Matangazo ya kibiashara

Chanzo kimoja kimeliambia shirika la habari la ufaransa AFP kuwa jeshi la Drc limekabiliana na wapiganaji waasi ambao walivamia ghala la tume ya uchaguzi wilayani beni siku chache baadaya ghala la CENI jijini kinshasa kuteketezwa kwa moto.

Afisa mkuu wa Tume ya uchaguzi ceni wilayani Beni Deogratias Mbayahi amesema ghala hilo limehifadhi mashine za kupigia kura takribani elfu mbili na vifaa vingine,na kuongeza kuwa hakuna kitakachobadilika kuhusu tarehe ya uchaguzi.

Hayo yanajiri wakati huu Ramazani shadari mgombea kiti cha uraisi nchini Congo dr kutoka vyama vinavyo muunga mkono raisi Joseph Kabila akiwasili mjini Goma mashariki mwa Congo kuendeleza kampeni zake.