DRC-EBOLA-AFYA

Chanjo dhidi ya Ebola yaanza kutolewa kwa wafanyakazi wa afya mashariki mwa DRC

Kituo kinachotoa huduma kwa wagonjwa wa Ebola (CTE) Mangina, Kivu Kaskazini, DRC.
Kituo kinachotoa huduma kwa wagonjwa wa Ebola (CTE) Mangina, Kivu Kaskazini, DRC. Florence Morice/RFI

Chanjo ya kuzuia maambukizi ya ugonjwa hatari wa Ebola imeanza kutolewa kwa wafanyakazi wa afya mjini Goma, katika mkoa wa Kivu Kaskazini, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Matangazo ya kibiashara

Wizara ya afya inasema, kuwa kati ya watu 207 ambao wamepewa chanjo hiyo katika mkoa wa Kivu Kaskazini, hakuna yeyote aliyeambukizwa kati yao.

Hatua hii imekuja, baada ya watu watatu waliokuwa wametokea Beni, kugundulika kuwa wameambukizwa Ebola wakiwa Goma wiki iliyopita.

Tangu mwezi Agosti, maambukizi haya yamesababisha vifo vya watu 313 katika Mkoa wa Kivu Kaskazini, hasa Wilayani Beni.