DRC-FDLR-FARDC-USALAMA

Jeshi la DRC lawashikilia viongozi wakuu wawili wa FDLR

Wanamgambo wa FDLR wajisalimisha katika kijiji cha Kateku mashariki mwa DRC, Mei 30 mwaka 2014.
Wanamgambo wa FDLR wajisalimisha katika kijiji cha Kateku mashariki mwa DRC, Mei 30 mwaka 2014. © REUTERS/Kenny Katombe

Viongozi wakuu wawili wa kundi la waasi wa Kihutu wa Rwanda (FDLR) linalopiga kambi mashariki mwa DRC wamekamatwa na jeshi la nchi hiyo (FARDC). Watu hao ni pamoja na msemaji wa FDLR, La Forge Fils Bayeze, na afisa anayehusika na upelelezi katika kundi hilo.

Matangazo ya kibiashara

Tangazo hilo lilitolewa Jumatatu, Desemba 17 na vikosi vya vya jeshi la DRC, FARDC, ambavyo vinasema kuwa viongozi wa kundi hilo la FDLR wamekamatwa Jumamosi wiki iliyopita.

Jeshi la DRC limebaini kwamba viongozi hao wa FDLR walikamatwa katika wilaya ya Bunagana katika eneo la Rutshuru, karibu na mpaka na Uganda.

Kwa mujibu wa msemaji mmoja wa FARDC katika jimbo la Kivu Kaskazini, Meja Guillaume Ndjike, operesheni hiyo iliendeshwa na kitengo cha upelelezi cha jeshi. Kwa upande mwingine, hakuna taarifa kuhusu wapi wanazuiliwa wawili hao.

Haijafahamika kama wamesafirishwa nchini Rwanda au bado wanaendelea kuzuiliwa nchini DRC ? Siwezi ni kathibitisha kati ya maswali hayo," amejibu Meja Guillaume Ndjike. "Tunahitaji maelezo yao," ameongeza. Lakini wapiganaji wote wa FDLR wanapaswa kurejeshwa Rwanda. Kitu ambacho Rwanda inaomba.

Siku ya Jumapili, Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda, Olivier Nduhungirehe, aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter: "Nina imani kuwa (La Forge Fils Bayeze) atarejeshwa nchini Rwanda." Akihojiwa na RFI, hata hivyo amesema hana taarifa kuhusu madai hayo.

Wawili hao kukamatwa ni pigo jingine kwa kundi la waasi wa Kihutu wa Rwanda, FDLR.

Mnamo mwezi Novemba, wapiganaji wa zamani zaidi ya mia moja na familia zao walifukuzwa kutoka kambi za wakimbizi za Kanyabayonga, Walungu na Kisangani, mashariki na kaskazini mwa DRC. Wote walirudishwa kwa nguvu nchini Rwanda.

Aidha, askari wawili wa DRC waliuawa baada ya kukamatwa kwa viongozi hawo wawili wa FDLR.