MADAGASCAR-UCHAGUZI-SIASA

Raia wa Madagascar kumchagua rais wao mpya katika duru ya pili

Wagombea wawili katika duru ya pili ya uchaguzi wa urais Madagascar, Andry Rajoelina (kulia) na Marc Ravalomanana (kushoto) tarehe 9 Desemba 2018.
Wagombea wawili katika duru ya pili ya uchaguzi wa urais Madagascar, Andry Rajoelina (kulia) na Marc Ravalomanana (kushoto) tarehe 9 Desemba 2018. Mamyrael / AFP

Raia wa Madagascar watapiga kura Jumatano wiki hii ikiwa ni duru ya pili ya uchaguzi utakaowakutanisha marais wawili wa zamani wa taifa hilo, Marc Ravalomanana na Andry Rajoelina.

Matangazo ya kibiashara

Inaelezwa kuwa huenda upinzani kati ya wawili hawa ukafufua sintofahamu zaidi ya kisiasa kwenye taifa hilo ikiwa upande mmoja utakataa kutambua matokeo.

Viongozi hawa wanaenda kwenye uchaguzi wa duru ya pili hapo kesho baada ya kuibuka wa kwanza na wapili katika uchaguzi wa duru ya kwanza mwezi Novemba.

Katika duru ya kwanza, Rajoelina alishinda kwa asilimia 39.23 huku mpinzani wake Ravalomanana, akimaliza wa pili kwa asilimia 35.55.