DRC-UCHAGUZI-USALAMA

Serikali ya DRC yatangaza hatua za kiusalama wakati wa uchaguzi

Wizara ya Mambo ya Ndani ya DRC imetangaza kuwa jeshi litasaidia polisi kuimarisha usalama wakati wa uchaguzi wa Desemba 23 (picha ya kumbukumbu).
Wizara ya Mambo ya Ndani ya DRC imetangaza kuwa jeshi litasaidia polisi kuimarisha usalama wakati wa uchaguzi wa Desemba 23 (picha ya kumbukumbu). KUDRA MALIRO / AFP

Baada ya wiki moja ya kampeni iliyogubikwa na matukio ya machafuko yaliyosababisha vifo vya watu kadhaa, Wizara ya Mambo ya Ndani imetangaza kwamba imechukuwa hatua za kiusalama kwa siku ya Uchaguzi Mkuu Desemba 23.

Matangazo ya kibiashara

Maofisa wawili wa polisi watakuwa katika kila moja ya vituo vya kupigia kura 75,000 kwa mujibu wa Waziri wa Mambo ya Ndani Henri Mova. Wengine watatumwa kwenye maeneo muhimu na pia kwenye mipaka ya nchi.

Kwa siku hiyo Mipaka yote ya nchi itafungwa.

Mipaka ya nchi kavu itafungwa kuanzia Jumamosi usiku wa manane hadi Jumapili usiku wa manane. Tunapaswa kujilinda na makundi ya watu wenye silaha kutoka nje ya nchi," amesema.

Jeshi la Congo pia litasaidia, lakini litakuwa mbali kabisa na maeneo ya kupigia kura moja kwa moja ya vituo vya kupigia kura, Waziri Mova ameahadi. "Polisi tu ndio wameruhusiwa kulinda moja kwa moja mchakato wa uchaguzi," ameongeza.

Hayo yanajiri wakati vita vya maneneo vimeanza kujitokea kati ya makundi mawili ya upinzani.

Baada ya muungano wa upinzani Lamuka unaowakilishwa na Martin Fayulu kueleza kwamba uko tayari kushiriki uchaguzi wa Jumapil bila matumizi ya machine za kupigia kura, muungano wa chama tawala unasema huo ni uamuzi wa watu ambao hawakusoma mazingira ya uchaguzi kabla ya kuingia kwenye kinyang’anyiro hicho.

Andre Alain Atundi msemaji wa chama tawala na washirika wake amesema hakika uamuzi huo ni wa mtu anaetapatapa.

Upande wake Felix Tshisekedi amesema Martin Fayule ni mgombea wa mkanganyiko na kwamba wapiga kura ndio wataoamuwa.

Haya yanajiri wakati zikibaki siku 5 tu kabla ya uchaguzi.