BURKINA FASO-UFARANSA-USHIRIKIANO-USALAMA

Ufaransa kuendelea kuisaidia kijeshi Burkina Faso

Rais wa Burkina Faso Roch March Christian Kaboré na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron katika ikulu ya Elysee, Desemba 17, 2018.
Rais wa Burkina Faso Roch March Christian Kaboré na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron katika ikulu ya Elysee, Desemba 17, 2018. © ludovic MARIN / AFP

Rais wa Burkinafso Jean Marc Kabore yuko ziarani nchini Ufaransa ambapo Jumatatu wiki hii amekutana kwanza na Waziri wa Majeshi ya Ufaransa Florence Parly kabla ya kukutana na mwenyeji wake Emmanuel Macron.

Matangazo ya kibiashara

Mazungumzo ya viongozi hao wawili yamelenga maswala ya usalama, ambapo Ufaransa na Burkina Faso wameongeza mkataba wa ulinzi kati ya serikali ili kuboresha mfumo wa kisheria wa ushirikiano wa kijeshi kati ya nchi hizo mbili.

Rais Kabore amesema vita dhidi ya ugaidi imepewa kipao mbele katika ushirikiano huo wa kijeshi.

Katika miezi ya hivi karibuni, kikosi cha jeshi la Ufaransa Afrika magharibi (Barkhane) kilitoa msaada mara kadhaa kwa jeshi la Burkina Faso katika kupambana na makundi ya wanamgambo wa Kiislamu.

Hata kama Paris haina nia ya kuimarisha uwepo wake wa kijeshi wakati huu nchini Burkina faso, hata hivyo tayari itasaidia Burkina Faso kwa mafunzo, ushauri na vifaa.

"Ufaransa itaendelea kusaidia, kwa ombi la serikali ya Burkina Faso, jitihada zinaendelea kwa mfumo wa usalama na sheria," amesema Rais Emmanuel Macron.