Wananchi wa DRC kupiga kura siku ya Jumapili

Sauti 14:01
Mgombea wa chama tawala nchini  Emmanuel Ramazani Shadary
Mgombea wa chama tawala nchini Emmanuel Ramazani Shadary Junior D. KANNAH / AFP

Wananchi wa DRC watapiga kura siku ya Jumapili, kumchagua rais mpya. Kampeni zinamalizika wiki hii kuelekea Uchaguzi huo wa kihistoria.

Matangazo ya kibiashara

Ushindani mkali ni kati ya wagombea watatu, Emmanuel Shadary kutoka chama tawala, Martin Fayulu kutoka muungano wa upinzani wa Lamuka, na Felix Tshisekedi.

Tume ya Uchaguzi CENI inasema iko tayari kwa uchaguzi huu licha ya kukabiliana na changamoto mbalimbali ikiweko kuteketea moto vya baadhi ya vifaa vya kupigia kura.