Fatoue Bensuda: ICC haitosita kuchukuwa hatua kwa watakaochochea machafuko DRC
Imechapishwa:
Mwendesha mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya ICC Fatoue Bensuda, ameonya kuwa hatosita kumchukulia hatua yeyote atakayesababisha mauaji ya kisiasa kipindi hiki cha kisiasa nchini DRC.
Bensuda amesema anafuatulia kwa karibu kinachoendelea nchini DRC, na kutoa wito kwa wanasiasa kuhakikishia kuwa hawachochei machafuko.
Watu saba wameripotiwa kupoteza maisha katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo hasa ngome za upinzani katika makabiliano na vikosi vya usalama.
Hayo yanajiri wakati tume huru ya Uchaguzi CENI imechukuwa uamuzi wa kuahirisha uchguzi uliokuwa umepangwa kufanyika Jumapili Desemba 23 hadi Desemba 30.
Wanasiasa nchini DRC wametofautiana kuhusu hatua hiyo, huku baadhi wakiona kuwa ni dalili ya kuwa uchaguzi huo utagubikwa na udanganyifu mkubwa.