DRC-SIASA-MAREKANI

Marekani yahimiza Uchaguzi huru na haki nchini DRC

Wagombea urais nchini  Emmanuel Ramazani Shadary, Félix Tshisekedi, Martin Fayulu.
Wagombea urais nchini Emmanuel Ramazani Shadary, Félix Tshisekedi, Martin Fayulu. Photos/Montage/RFI

Balozi mpya wa Marekani nchini DRC Mike Hammer amehimiza Uchaguzi huru, haki, na utakaominika Jumapili ijayo. 

Matangazo ya kibiashara

Hammer amesema, iwapo uchaguzi huo utakwenda vema, utasaidia kuimarisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

Uchaguzi huo ulikuwa umepangwa kufanyika leo lakini ukaahirishwa hadi Jumapili ijayo, baada ya moto kuteketeza vifaa vya kupigia kura jijini Kinshasa.

Zaidi ya wagombea 20 wanawania urais lakini ushindani ni kati ya mgombea wa chama tawala Emmanuel Shadary, Martin Fayulu kutoka muungano wa upinzani Lamuka na Felix Tshisekedi.

Wananchi wengi wa DRC walikuwa na matumaini ya kupiga kura, na kuahirishwa kwa uchaguzi huo kuliwakasirisha huku baadhi ya wapinzani wakisema kilichofanyika ni mbinu ya serikali kuchelewesha Uchaguzi huo.