DRC-MONUSCO-UCHAGUZI-SIASA

MONUSCO: Tuko tayari kusaidia katika mchakao wa uchaguzi

Ceni ilitangaza Alhamisi Desemba 20, 2018 kusogezwa mbele kwa wiki uchaguzi nchini DRC.
Ceni ilitangaza Alhamisi Desemba 20, 2018 kusogezwa mbele kwa wiki uchaguzi nchini DRC. Caroline Thirion / AFP

Wananchi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, sasa wanatarajiwa kupiga kura siku ya Jumapili Desemba 30, kumchagua rais mpya na viongozi wengine.

Matangazo ya kibiashara

Uchaguzi huo ambao umesubiriwa tangu mwaka 2006, ulitarajiwa kufanyika Jumapili iliyopita lakini ukaahirishwa kwa wiki moja zaidi ili Tume ya Uchaguzi imemalize maandalaizi yake.

Wagombea wa urais, wameingia katika wiki ya mwisho ya kutafuta kura, wakati huu Umoja wa Mataifa ukisema kuwa utakuwa tayari kusaidia, ili kufanikisha zoezi hili.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limesema ucheleweshwaji huu utasaidia kuweka mazingira ya Uchaguzi huo kuwa huru na haki.