Wananchi wa DRC, wanatarajiwa kupiga kura siku ya Jumapili kumchagua rais mpya na viongozi wengine, baada ya zoezi hilo kuahirishwa kwa wiki moja baada ya kuteketea kwa jengo la kuhifadhi vifaa vya kupigia kura jijini Kinshasa. Tunajadili hili, tukiwa na Steven Chondo, mmoja wa maafisa wa kampeni wa mgombea wa chama tawala Emmanuel Shadary, lakini pia Reubens Mikindo , Naibu Katibu Mkuu wa chama kikuu cha upinzani UDPS, ambacho mgombea wake ni Felix Tshisekedi.