Pata taarifa kuu
SUDAN-MAANDAMANO-UCHUMI

Polisi yazima maandamano kuelekea ikulu ya rais Khartoum

Waandamanaji katika mji wa Khartoum, Sudan, Desemba 25, 2018.
Waandamanaji katika mji wa Khartoum, Sudan, Desemba 25, 2018. REUTERS / Mohamed Nureldin Abdallah
Ujumbe kutoka: RFI
Dakika 1

Waandamanaji nchini Sudan Kusini, wameendelea kujitokeza katika miji mbalimbali hasa jijini Khartoym kulalamikia kupanda kwa bei ya mkate na mafuta.

Matangazo ya kibiashara

Polisi wa kupambana na ghasia jana walitumia mabomu ya jkutoa machozi na maji ya kuwasha, jijini Khartoum kukabilana na waandamanaji hao ambao pia wanmataka rais Omar A Bashir ajiuzulu.

Waandamanaji wamesikika wakisema, uhuru, amani, haki na mapinduzi ndio kitu wanachokitaka.

Maandamano hayo yanatarajiwa kuendelea leo na rais Bashir ameonya kuwa atakuja na mikakati ya kumaliza maandamano hayo.

Hayo yanajiri wakati shirika la haki za binadamu la Amnesty International limebaini kwamba waandamanaji thelathini na saba "waliuawa kwa kupigwa risasi" na vikosi vya usalama katika kipindi cha siku tano za maandamano dhidi ya hali ngumu ya maisha nchini humo.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.