DRC-SIASA-MAANDAMANO

DRC: Wakazi wa Beni waandamana kupinga hatua ya CENI

Jeshi la DRC (FARDC) laimarisha ulinzi katika mji wa katika Beni ukikaribia uchaguzi wa urais wa Desemba 30, 2018.
Jeshi la DRC (FARDC) laimarisha ulinzi katika mji wa katika Beni ukikaribia uchaguzi wa urais wa Desemba 30, 2018. REUTERS/Goran Tomasevic

Jeshi na polisi wamezima maandamano ya wakazi wa Beni waliokuwa wameingia mitaani kupinga hatua ya Tume Huru ya Uchaguzi (CENI) ya kuahirisha uchaguzi katika maeneo ya Beni, Butembo (mashariki mwa DRC) na Yumbi (magharibi mwa nchi).

Matangazo ya kibiashara

Vikosi vya usalama na ulinzi vimetumia mabomu ya machozi kwa kuwatawanya waandamanaji ambao walishambulia vituo vya matibabu ya ugonjwa hatari wa Ebola katika mji wa Beni. Uchaguzi nchini DRC uliokuwa umepangwa kufanyika Jumapili Desemba 23 uliahirishwa kwa mara ya kwanza hadi Desemba 30.

Tume ya Uchaguzi (CENI) ilitangaza siku ya Jumatano kwamba imeahirisha uchaguzi katika mji wa Beni na pia katika eneo jirani la Butembo kwa sababu ya ugonjwa wa Ebola. Uchaguzi pia umefutwa kufanyika Jumapili na kuahirishwa katika mji wa Yumbi,magharibi mwa nchi, ambapo ghasia za kikabila zilisababisha mamiaya raia kuuawa wiki moja iliyopita.Miji hii inajulikana kuwa ni ngome za upinzani dhidi ya Rais Joseph Kabila. Kwa mujibu wa wanasiasa, CENI imechukua uamuzi huu kwa kutaka Emmanuel Shadary Ramazani, mgombea anayeungwa mkono na Joseph Kabila aweze kupata kura nyingi na hivyo kutangazwa mshindi.

"Kundi la waandamanaji lilitaka kuingia katika ofisi ya CENI (...) ili kuomba uamuzi huo ufutwe," amesema Giscard Yere, mkazi wa Beni. "Lakini polisi na askari waliokuwa eneo hilo walitawanya waandamanaji. "