DRC-SIASA-USALAMA

Hatua ya Ceni ya kuahirisha uchaguzi katika maeneo matatu DRC yazua sintofahamu

Makao makuu ya Tume Huru ya Uchaguzi DRC (CENI), Kinshasa.
Makao makuu ya Tume Huru ya Uchaguzi DRC (CENI), Kinshasa. JOHN WESSELS / AFP

Hatua ya tume ya uchaguzi nchini DRC CENI, kutangaza kuahirishwa kwa uchaguzi wa rais na ule wa wabunge wa majimbo na Kitaifa kwenye maeneo ya Beni na Butembo pamoja na Yumbi magharibi mwa nchi hiyo hadi mwezi Machi mwaka 2019 imeendelea kuzua hali ya wasiwasi na huenda ikaathiri pakubwa hali ya usalama.

Matangazo ya kibiashara

Tume ya Uchaguzi imetetea uamuzi wake kufuatilia kile inachosema ni kwa sababu ya ugonjwa hatari wa Ebola pamoja na makundi ya wapiganaji wenye silaha wanaoendelea kutishia usalama.

Iwapo uamuzi wa Ceni utatekelezwa wapiga kura takriban 1,256,177 kutoka (Beni = 675.600, Beni mjini = 182.800, Butembo mjini = 330.744, Butembo mjini = 330.744) hawatoshiriki uchaguzi huo.

Uamuzi huu umewakarisha wanasiasa wa upinzani, ambao wanasema maeneo hayo ni ngome zao.

Mbali na taarifa hiyo, tume huru ya Uchaguzi Ceni imetangaza kuwa matokeo ya uchaguzi huu wa Jumapili yatatangazwa tarehe 15 na rais mpya kuapishwa tarehe 18 mwezi Januari, suala ambalo linaacha maswali kuhusu maeneo ambayo hayapiga kura.