MADAGASCAR-UCHAGUZI-SIASA

Madagascar: Rajoelina atangazwa mshindi wa uchaguzi wa urais

Andry Rajoelina ameshinda uchaguzi wa urais nchini Madagascar, kulingana na matokeo rasmi ya muda yaliyotolewa na Tume ya Uchaguzi.
Andry Rajoelina ameshinda uchaguzi wa urais nchini Madagascar, kulingana na matokeo rasmi ya muda yaliyotolewa na Tume ya Uchaguzi. © REUTERS/Malin Palm

Rais wa zamani wa Madagascar Andry Rajoelina ameshinda uchaguzi wa urais wa Desemba 19, kulingana na matokeo rasmi ya muda yaliyotolewa na Tume ya Kitaifa ya Uchaguzi.

Matangazo ya kibiashara

Andry Rajoelina, aliyewahi kuwa rais wa mpito, ameshinda uchaguzi kwa 55.66% ya kura. Mpinzani wake Marc Ravalomanana amepata 44.34% ya kura.

Andry Rajoelina, mwenye umri wa miaka 44, ni maarufu sana kwa wawanchi wa Madagascar, kwa kuwa aliwahi kuwa meya wa mji mkuu mwaka 2007 na aliongoza nchi kwa miaka 5, kuanzia 2009 hadi 2013.

Rajoelina amesema "Andry Rajoelina wa mwaka 2018, sio Andry Rajoelina wa mwaka 2009. Nimepiga hatua kubwa. Nimebadilika. Nimejiandaa na niko tayari sasa!

Mahakama Kuu ya Katiba sasa ina siku tisa kutangaza matokeo ya mwisho.