Pata taarifa kuu
BURUKINA FASO-USALAMA

Polisi kumi wauawa katika shambulizi Burkina Faso

Maafisa wa polisi wa Burkina Faso kwakati wa mazishi ya wenzao watatu, Mei 21, 2016 Ouagadougou.
Maafisa wa polisi wa Burkina Faso kwakati wa mazishi ya wenzao watatu, Mei 21, 2016 Ouagadougou. AHMED OUOBA / AFP
Ujumbe kutoka: RFI
1 Dakika

Maafisa 10 wa polisi wameuwa na wengine watatu kujeruhiwa baada ya kushmabuliwa na magaidi Kaskazini Magharibi mwa nchi ya Burkina Faso.

Matangazo ya kibiashara

Ripoti zinasema kuwa, gari la maafisa hao wa polisi lilishambuliwa, wakati likipiga doria katika eneo hilo karibu na mpaka wa nchi ya Mali.

Polisi walikwenda katika eneo hilo, baada ya watu wenye silaha kuvamia shule moja na kuteketeza moto vitabu vya wanafunzi.

Shambulio hilo linatokea siku chache baada ya Ufaransa kutangaza kwamba itaendelea kuisaidia kijeshi Burkina Faso.

"Ufaransa itaendelea kusaidia, kwa ombi la serikali ya Burkina Faso, jitihada zinaendelea kwa mfumo wa usalama na sheria," amesema Rais Emmanuel Macron.

Katika miezi ya hivi karibuni, kikosi cha jeshi la Ufaransa Afrika magharibi (Barkhane) kilitoa msaada mara kadhaa kwa jeshi la Burkina Faso katika kupambana na makundi ya wanamgambo wa Kiislamu.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.