DRC-EU-SIASA-USALAMA-USHIRIKIANO

Umoja wa Ulaya walaani hatua ya DRC kumfukuza balozi wake

Uhusiano wa Kinshasa na Umoja wa Ulaya waendelea kudorora. Rais Kabila anyooshewa kidole cha lawama kusababisha hali hiyo
Uhusiano wa Kinshasa na Umoja wa Ulaya waendelea kudorora. Rais Kabila anyooshewa kidole cha lawama kusababisha hali hiyo REUTERS/Yves Herman/File Photo

Umoja wa Ulaya, umelaani hatua ya serikali ya DRC kumfukuza Balozi wake nchini humo, hatua ambayo umoja huo unasema haikubaliki na hakukuwa na sababu ya kufanya hivyo.

Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Mambo ya nje wa DRC Leonard She Okitundu amesema Balozi huyo Bart Ouvry, raia Ubelgiji ana saa 48 kuondoka nchini humo, na ni uamuzi unakuja, siku mbili kuelekea Uchaguzi wa Jumapili.

Hatua hii ya DRC imeonekana kama kulipiza kisasi kwa Umoja wa Ulaya, kwa kuendelea kumwekea vikwazo Emmanuel Ramazani Shadary mgombea wa urais kupitia chama tawala.

Mchakato wa uchaguzi nchini DRC umeanza kuingiliwa na disari, baada ya gavana wa mkoa wa Kinshasa kutoa uamuzi wa kusitisha kampeni katika mji huo na siku mbili baada ye CENI kuchukuwa uamuzi wa kuahirisha uchaguzi katika maeneo ya Beni, Butembo (Mashariki mwa DRC) na Yumbi (Magharibi mwa nchi).

Hali hiii imezua wasiwasi mgubwa nchini humo. Tayari muungano wa upinzani nchini DRC Lamuka unaowakilishwa na mgombea urais Martin Fayulu, umetoa wito wa maandamano na mgomo wa siku nchi nzima kupingwa kuahirishwa kwa Uchaguzi katika maeneo ya ya Beni, Butembo na Yumbi.