SUDAN-MAANDAMANO-UCHUMI

Maandamano Sudan: Rais Al-Bashir atoa wito kwa polisi kujizuia

Rais wa Sudan Omar al-Bashir wakati akikutana na maofisa wakuu wa polisi Khartoum siku ya Jumapili (Desemba 30).
Rais wa Sudan Omar al-Bashir wakati akikutana na maofisa wakuu wa polisi Khartoum siku ya Jumapili (Desemba 30). © ASHRAF SHAZLY / AFP

Baada ya siku 10 za maandamano nchini Sudan, na kusababisha vifo vya watu wasiopungua 19, Rais wa Sudan amewataka polisi kujizuia na kutotumia nguvu za kupita kiasi dhidi ya waandamanaji.

Matangazo ya kibiashara

Siku ya Jumapili Rais Omar al-Bashir alizungumza kwa upole mbele ya viongozi wakuu wa polisi. Kutokana na maandamano yanayoendelea kushika kasi kufuatia kuongezeka mara dufu kwa bei ya mkate na bei ya mafuta ya dizeli, rais wa Sudan aliwaambia polisi wake: "Tunataka kudumisha usalama na tunataka polisi kufanya hivyo kwa kutumia nguvu kidogo. "

Kauli hii inakuja baada ya watu 19 kupoteza maisha katika "matukio ya uporaji," kwa mujibu wa serikali.

Kwa upande wake, shirika la kimataifa la Haki za Binadamu la Amnesty International limebaini kwamba watu wasiopungua 37 waliuawa wakati wa maandamano hayo. Amnesty International inamomba, kama Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, uchunguzi huru kuhusu mauaji hayo.

Kama ishara ya kuondokana na maandamano, rais wa Sudan pia amekiri kuwa Sudan inakabiliwa na matatizo ya kiuchumi: "Tunatambua kuwa tuna matatizo ya kiuchumi, lakini hayawezi kutatuliwa kwa machafuko, uharibifu, uporaji na wizi," Rais Omar al- Bashir amesema.

Ameonya wale wenye ndoto za mapinduzi, akisema: "Hatutaruhusu raia wetu kuwa wakimbizi."