DRC-SIASA-USALAMA

Uchaguzi DRC: Huduma ya intaneti na mitandao ya kijamii yafungwa DR Congo

Wanachama wa Tume ya Uchaguzi (CENI) wakiendelea kuhesabu kura baada ya uchaguzi mjini Kinshasa tarehe 30 Desemba 2018.
Wanachama wa Tume ya Uchaguzi (CENI) wakiendelea kuhesabu kura baada ya uchaguzi mjini Kinshasa tarehe 30 Desemba 2018. REUTERS/Baz Ratner

Huduma ya intaneti na mitandao ya kijamii imefungwa katika miji mbalimbali nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo siku moja tu baada ya uchaguzi mkuu uliofanyika Jumapili Desemba 30.

Matangazo ya kibiashara

Upinzani unashtumu serikali kutoa uamuzi wa kufungwa kwa huduma ya intaneti na mitandao ya kijamii ili kukataa aibu ya kushindwa kwa mgombea wa muungano wa chama tawala Emmanuel Ramazani Shadary.

Hata hivyo zoezi la kuhesabu kura linaendelea, huku katika mji wa Goma, katika mkoa wa Kivu Kaskazini, Mashariki mwa nchi zoezi hilo limemalizika tangu jumatatu jioni.

Wawakilishi wa Vodacom pia wamesema kuwa serikali iliwaagiza kufunga mawasiliano ya intaneti, kwa mujibu wa shirika la Habari la AFP. Lakini Waziri wa mawasiliano nchini humo Emery Okundji amesema kuwa hajui kuhusu hali hiyo.

Wagombea wakuu wa upinzani ni Martin Fayulu na Felix Tshisekedi.

Hali ya sintofahamu bado inaendelea katika baadhi ya maeneo nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.