SUDAN-MAANDAMANO-BASHIR-SIASA

Rais wa Sudan aagiza kuundwa kwa jopo la kuchunguza machafuko

Rais Omar Al Bashir katika hotuba yake ya mwaka mpya jijini Khartoum Desemba 31 2018
Rais Omar Al Bashir katika hotuba yake ya mwaka mpya jijini Khartoum Desemba 31 2018 ASHRAF SHAZLY | AFP

Rais wa Somalia Omar al-Bashir ameunda jopo maalum kuchunguza na kupata taarifa za kina kuhusu maandamano yanayoendelea kulalamikia kupanda kwa bei ya mkate lakini pia kushinikiza kujiuzulu kwake.

Matangazo ya kibiashara

Maandamano hayo yaliyoanza kushuhudiwa mwezi Desemba mwaka 2018, yamesababisha vifi vya watu 19, huku mamia wakijeruhiwa na wengine kutiwa mbaroni na maafisa wa usalama.

Idadi kubwa ya mauaji yametokea katika jiji kuu Khartoum tangu, harakati za kushinikiza mabadiliko hayo baada ya mkate kupanda bei mara tatu zaidi.

Hata hivyo, Shirika la Kimataifa la kutetea haki za vindamu la Amnesty International linasema kuwa idadi ya watu waliopoteza maisha ni 37.

Waandaji wa maandamano hayo wanasisitiza kuwa yataendelea hadi pale matakwa yao yatakaposikilizwa na serikali ya Khartoum.