MALI-MAUAJI-WAFUGAJI-WAKULIMA

Watu 37 wauawa nchini Mali katika mapigano ya kikabila

Kijiji cha Peul kulikotokea mashambulizi nchini Mali
Kijiji cha Peul kulikotokea mashambulizi nchini Mali © Coralie Pierret / RFI

Raia 37 wameuawa baada ya watu wenye silaha wanaoaminiwa kuwa wawindaji kutoka jamii ya Dogon kuvamia wafugaji wa jamii ya Fulani nchini Mali. 

Matangazo ya kibiashara

Ni mauaji mabaya kuripotiwa mwanzoni mwa mwaka 2019, kati ya jamii hizi mbili, Fulani na Dogon ambazo zimekuwa zikizozana kwa muda mrefu.

Serikali jijini Bamako inasema, inahofia kuwa huenda idadi ya vifo ikaongezeka kwa sababu, raia wengi walijeruhiwa katika uvamizi huo.

Mbali na vifo na majereha, nyumba za wafugaji hao ziliteketezwa moto, na kuwafanya kukosa mahali pa kulala.

Inaelezwa kuwa chanzo cha mafuko hayo ni tuhma kuwa wafugaji wa jamii ya Fulani wamekuwa wakienda kuchunga ng'ombe zao katika mashamba ya jamii ya Dogon.

Mwaka uliopita, watu zaidi ya 500 walipoteza maisha katika machafuko kati ya jamii hizo mbili.