SENEGAL-SALL-SIASA-HAKI

Mahakama Kuu yafutilia mbali rufaa ya meya wa zamani wa Dakar Khalifa Sall

Picha kubwa ya meya wa zamani wa mji mkuu wa Senegal, Dakar, Khalifa Sall.
Picha kubwa ya meya wa zamani wa mji mkuu wa Senegal, Dakar, Khalifa Sall. SEYLLOU / AFP

Mahakama Kuu ya Senegal imefutilia mbali madai ya meya wa zamani wa Dakar Khalifa Sall ambaye amekuwa anapinga hukumu ya kifungo cha miaka mitano jela kwa kosa la utapeli. Hatua hii imetolewa ikiwa imesalia miezi miwili kabla ya uchaguzi wa urais ambao Khalifa Sall atawania.

Matangazo ya kibiashara

Mahakama "inafutilia mbali madai ya Khalifa Ababacar Sall" ambayo "haikubaliki na haina msingi," amesema Jaji mkuu wa Mahakama Kuu, Amadou Baal.

Upande wa utetezi wa Khalifa Sall, mmoja kati wapinzani wakuu wa Rais Macky Sall katika uchaguzi wa urais uliopangwa kufanyika Februari 24, ametangaza kwamba atakataa rufaa dhidi ya uamuzi huo wa Mahakama ya Kuu.

Mara baada ya kujulishwa uamuzi, tutaanzisha utaratibu mwengine wa kisheria", utaratibu ambao utaruhusu pande husika kupinga uamuzi uliochukuliwa katika ngazi ya Mahakama Kuukama kutakuwa na" hitilafu ya wazi "amewaambia waandishi mmoja wa wanasheria wa Khalifa Sall, Seydou Diagne.

Khalifa Sall, 62, ambaye anazuiliwa kwa karibu miaka miwili sasa, anaendelea kusalia kwenye kinyang'anyiro cha urais, wamesema wafuasi wake.

"Mahakama imekataa rufaa zote" laikini "hajaweza kumzuia Khalifa Sall kutekeleza haki zake za kiraia. Hadi leo hii, bado ana haki zote za kiraia, kupiga kura na kuwania katika uchaguzi," amesema mwanasheria wake mwingine, Amadou Ali Kane , wakati wengi wa wafuasi wa meya wa zamani wa mji mkuu wa Dakar wamekuwa wakiandamana karibu na Mahakama Kuu, ambayo iko chini ya ulinzi mkali wa polisi.