NIGERIA-BOKO HARAM-USALAMA

Askari watano wapoteza maisha katika ajali ya helikopta ya jeshi Nigeria

Askari wa jeshi la Nigeria katika vita na makundi ya magaidi.
Askari wa jeshi la Nigeria katika vita na makundi ya magaidi. Reuters

Jeshi la Nigeria limepoteza askari wake watano waliopteza maisha katika ajali ya helikopta ya jeshi iliyoanguka wakati ilikuwa ikitoa msaada wa kijeshi kwa kambi ya jeshi iliyokuwa inashambuliwa na kundi la Boko Haram, Kaskazini Mashariki mwa Nigeria, Jeshi limetangaza.

Matangazo ya kibiashara

"Ni kwa masikitiko makubwa na huzuni ninatangaza vifo vya askari wetu watano waliokuwa wakisafiri katika helikopta ya jeshi ya Nigeria, Air Force, ambayo ilianguka wakati wa mapigano jana (Alhamisi)", Ibikunle Daramola, msemaji wa kikosi cha jeshi la wanaanga la Nigeria, amesema.

Marubani, mafundi na askari maafisa wawili ni miongoni mwa askari waliopoteza maisha.

Helikopta hiyo ilianguka wakati ilikuwa ikitoa msaada wa kijeshi kwa bataliani ya`1` 145 wakati wa shambulio dhidi ya kambi ya jeshi huko Damasak katika Jimbo la Borno, Kaskazini Mashariki mwa Nigeria. Shambulio lililoendeshwa na kundi la Boko Haram.

Wapiganaji wa Boko Haram wameongeza mashambulizi yao dhidi ya jeshi huko Borno na Yobe katika miezi ya hivi karibuni na kuua askari kadhaa.

Katika wiki moja tu, Boko Haram imeendesha mashambulizi manne katika kambi za kejeshi na vituo vya ukaguzi, ikiwa ni pamoja na kambi ya kijeshi ya Damasak.

ISWAP imedai kuwa ndio ilifanya mashambulizi haya, na kudai kuwaua askari 14 na kumshikilia mateka mwingine mmoja, kulingana na kituo cha Marekani cha Ufuatiliaji maalum wa wanamgambo wa Kiislamu (SITE).