DRCUNSC-SIASA-USALAMA

Tume ya uchaguzi DRC yajikanganya kwa kauli zake

Mwenyekiti wa CENI DRC, Corneille Nangaa, Novemba 5, 2017 Kinshasa
Mwenyekiti wa CENI DRC, Corneille Nangaa, Novemba 5, 2017 Kinshasa © JOHN WESSELS / AFP

Siku mbili tu kabla ya kutangazwa kwa matokeo ya awali ya uchaguzi mkuu wa rais wabunge la kitaifa na wa Mikoa nchini DRCongo, Tume huru huru ya uchaguzi CENI imesema asilimia 20 ya kura tayari zimekwisha hesabiwa.

Matangazo ya kibiashara

Tume huru ya Uchaguzi ambayo hapo awali ilikuwa imetangaza kuwa huenda ikaahirisha kutangaza matokeo ya uchaguzi Januari 6, imesema licha ya matatizo ilionayo kwa sasa katika zoezi la uhesabuji kura, matokeo hayo ya awali yatatangazwa kama ilivyopangwa.

Hayo yanajiri wakati huu Baraza Kuu la Maaskofu wa Kanisa Katoliki nchini humo likisema kwamba linafahamu mshindi wa uchaguzi huo na kuitaka Tume Huru ya uchaguzi (CENI) kutangaza matokeo ya ukweli na kisheria.

Baraza la maaskofu wa kanisa katoliki ambalo limekuwa likikosolewa na serikali ya DRC, kwa kuingilia kati maswala ya siasa hususan kwa kuwa waangalizi wa uchaguzi.

Katika hatua nyingine ripota wa RFI jijini Kinshasa Florence Maurice ambae alinyang’anywa kibali cha kufanya kazi nchini DRCongo amezuiliwa kuondoka nchini humo wakati huu Matangazo ya Radio France Intertenationale yakiwa hayasikiki baada ya kuzimwa mitambo kote nchini.