DRC-MAREKANI-SIASA-USALAMA

Uchaguzi DRC: Marekani yaionya Tume ya Uchaguzi DRC

Makao makuu ya Tume Huru ya Uchaguzi DRC (CENI), Kinshasa.
Makao makuu ya Tume Huru ya Uchaguzi DRC (CENI), Kinshasa. JOHN WESSELS / AFP

Marekani imetoa wito kwa Tume ya Uchaguzi (CENI) "kuheshimu" chaguo la wananchi wa DRC ambao walipiga kura kwa kumchagua rais mpya, kutangaza matokeo "sahihi".

Matangazo ya kibiashara

"Wale ambao watadhoofisha mchakato wa uchaguzi, kutishia amani, usalama au utulivu wa DRC, au kunufaika na rushwa hawatakubaliwa kuingia tena nchini Marekani au watakataliwa katika kunufaika na mfumo wa kifedha wa Marekani" wizara ya mambo ya nje ya Marekani imeonya.

Wakati huo huo Tume huru ya Uchaguzi ambayo hapo awali ilikuwa imetangaza kuwa huenda ikaahirisha kutangaza matokeo ya uchaguzi Januari 6, imesema licha ya matatizo ilionayo kwa sasa katika zoezi la uhesabuji kura, matokeo hayo ya awali yatatangazwa kama ilivyopangwa.

Hayo yanajiri wakati huu Baraza Kuu la Maaskofu wa Kanisa Katoliki nchini humo likisema kwamba linafahamu mshindi wa uchaguzi huo na kuitaka Tume Huru ya uchaguzi (CENI) kutangaza matokeo ya ukweli na kisheria.

Baraza la maaskofu wa kanisa katoliki ambalo limekuwa likikosolewa na serikali ya DRC, kwa kuingilia kati maswala ya siasa hususan kwa kuwa waangalizi wa uchaguzi.